Mabingwa watetezi wa kombe la muungano Kijitonyama Chipukizi SC wameyaanza vibaya mashindano hayo kwa kufungwa goli 2-1 na Kijitonyama Veterans, mchezo uliochezwa katika uwanja wa Bora Kijitonyama jijini Dar es salaam.

Wachezaji wa Kijitonyama Chipukizi wakingoja mawaidha toka kwa mwalimu wao
Katika mchezo huo Chipukizi walikuwa wa mwanzo kupata goli katika dakika ya 27 baada ya kuwakosa katika dakika za mwanzo kupitia kwa Seba ambaye aliwapa wakati mgumu walinzi wa Veteran katika kipindi cha Kwanza.
Katika kipindi cha kwanza Chipukizi walitawala eneo la kati huku kukichochewa na ufundi wa kijana aliyevalia uzi namba 11, ambaye alikuwa anavika mahali anapo hitajika kwa wakati huku akiichezesha vyema Chipukizi.
Veterani walisawazisha goli katika kipindi cha pili baada ya Chipukizi kuwaangaisha vilivyo Veteran na kupelekea Veteran kutumia mabavu na kuwachezea faulo wachezaji wa Chipukizi huku Mwamuzi akipeta baadhi ya faulo.
Baada ya Veterani kupata goli la kusawazisha, Kocha wa Chipukizi alienda kumweeleza kamisaa wa mchezo namna mwamuzi anapoelekea kuharibu mpambano kwa kushindwa kuwalinda wachezaji wake ambao wengi wao ndio nyota wanaotegemewa baadae.

Wachezaji wa Veterans wakisikiliza mawaiza
Veterans walipata goli lao la ushindi katika dakika za lala salama kwa mkwaju wa penati uliopigwa na mchezaji aliyetokea benchi.
Mpaka kipenga cha mwisho kinapulizwa Kijitonyama Chipukizi 1-2 Kijitonyama Veterans.






0 comments:
Post a Comment