vilabu

MIRAJI AENDA KUZIPA PENGP LA SWEDI ALIYEENDA KUZIPA PENGO LA NYOSSO

Beki wa Simba SC Miraji Adam aliyejiunga na Coastal union kuchukuwa nafasi ya Tumba Swedi
Wakati kukiwa na taarifa ya kufukuta upya sakata la beki wa Mbeya city Juma Nyosso dhidi ya Mshambuliaji wa Azam FC John Bocco, Mbeya city wameamu kumsajili beki kisiki wa Coastal union ya Tanga, nao Coastal wakajofoa beki kutoka Simba SC.

Coastal union katika hali ya kuhakikisha kikosi chake kinakuwa imara wamemsajili beki wa Simba SC Miraji Adam kwa mkopo wa miezi 6 baada ya kuitumikia Mtibwa sugar kwa Mkopo mwanzoni mwa msimu huu.

Miraji Adam ni miongoni mwa wachezaji walio tamba na Simba B iliyokuwa chini ya kocha Suleiman Matola amesema kuwa amejiunga na Coastal union ili apate nafasi zaidi ya kucheza.

''Nimekaa nje muda mrefu baada ya Simba kushindwa kuvunja mkataba wangu na sasa wamenipeleka kwa mkopo Coastal Union jambo ambalo nisingeweza kukataa. Nataka kumalizia mkataba wangu ndipo nijue mengine.

''Mpira ndiyo ajira yangu hivyo ni lazima nijitume kuhakikisha narudi katika kiwango changu cha mwanzo, naweza kusema Coastal ni mahali pazuri kwangu,'' alisema Miraji.
Beki Tumba Swedi akimwaga wino wa kuitumikia Mbeya city
Beki aliyechipukia katika kikosi cha Azam Academy na kwenda kuwa nguzu muhimu katika kikosi cha Coasta union ya Tanga Tumba Swedi amejiunga na Mbeya city kwenda kuimarisha safu ya ulinzi ya kikosi hicho kilicho pata pigo la kufungia kwa nahodha wake na beki wake kisiki Juma Nyoso.

Kwa taarifa iliyowekwa kwenye mtandao wa Mbeya city zinasema:
Aliyekuwa mlinzi wa kutumainiwa wa timu ya Coastal Union ya Tanga, Tumba Swedi Luo amejiunga na kikosi cha Mbeya City Fc.

Mapema leo kwenye ofisi la City zilizopo  jengo la Mkapa Hall jijini hapa Swedi ametia sini kandarasi ya mwaka mmoja na nusu tayari kabisa  kuitumikia timu yake mpya kwenye ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara na pia mashindano mengine.

Akizungumza mara baaada ya kutia saini kandarasi hiyo Swedi alisema kuwa amefurahi kujunga na timu ambayo imekuwa na hamasa kubwa kwenye mpira wa Tanzania bara tangu aliponda ligi kuu huku akiahidi kufanya kazi kwa uwezo wake wote aliojaaliwa na Mungu kwa lengo la kuisaidia City kupata mafaniio zaidi kwenye ligi kuu.

“Nimefurahi kujiunga na City, hii ni timu ambayo imekuwa na hamasa kubwa, tangu ilipopanda daraja imeleta changamoto nzuri na zaidi imekuwa timu ya ushindani na kutafuta mafanikio, hakika namshukuru mwenyezi mungu, hapa ni sehemu ambayo naweza kupata mafanikio zaidi, imani yangu kubwa ushirikino wa pamoja na niliowakuta hapa tutakuwa na mafanikio zaidi ya yale niliyokuta” alisema.

Tumba Swedi Luo kabla ya kujiunga na City alikuwa mchezaji wa Coastal Union kwa misimu miwili mfululizo  akicheza jumla michezo michezo  36 na kuisaidia  timu yake  hiyo ya zamani kushika nafasi tano kwenye msimamo wa ligi kuu ya vodacom msimu uliopita.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.