basketball

Migogoro ndiyo inayo didimiza kikapu

Brown Msyani
 

MGOGORO wa chama cha mpira wa kikapu mkoa wa Dar es Salaam (BD) umesababisha hali ya uwajibikaji kupungua katika bodi ya uongozi wa chama hicho, hali ambayo imesababisha kuwa na mapungufu katika kazi zake za kila siku.

Uchunguzi uliofanywa umebaini kuwa uongozi wa chama hicho umegawanyika katika makundi mawili, ambapo rais wake, Afred Ngalalija anafanya kazi peke yake bila ya kushirikiana na bodi ya chama hicho.

Pia imebainika kuwa Bodi ya BD inafanya kazi peke yake bila ya kumshirikisha rais aliyejiengua baada ya kuunda Kamati ya wadau wa mchezo wa kikapu, ambayo ilipingwa na bodi hiyo kwa madai haipo kikatiba.

Mkurugenzi wa Masoko wa BD,  Francis Ngomba alisema kwamba  Ngalalija alikiuka katiba ya BD ya utendaji wa kazi,  jambo ambalo lilijadiliwa katika mkutano wa viongozi wa klabu uliofanyika katika ofisi za mkuu mkoa wa Dar es Salaam Agosti 3 mwaka huu.

Alisema mkutano huo ulisimamiwa na afisa wa michezo mkoa wa Dar es Salaam, Adolf Ally pamoja na mwakilishi wa Shirikisho la kikapu Tanzania (TBF), Michael Maluwe na upande wa bodi ya BD walikuwapo aliyekuwa raisi wa chama hicho Ngalalija, Richard Jules (Makamu wa rais), Mohamed Tajiri (Mkurugenzi Mtendaji) na Francis Ngomba (Mkurugenzi wa masoko).

Wengine ni Jimmy Mkongo (Mkurugenzi wa ufundi na mashindano), Agnela Semwaiko (Mkrugenzi wa shule na watoto),  Robert Mnyerere (Mkurugenzi wa makocha) na Judith Ilunda (Mkurugenzi wa wanawake).

Akizungumzia kwa nini aliunda Kamati ya wadau wa mchezo wa kikapu, Ngalalija alisema alifanya hivyo baada ya BD kushindwa kuwalipa waamuzi sh 2,860,000 yakiwa ni malipo ya waamuzi kwa uchezeshaji wa ligi ya mpira wa kikapu ya RBA.

Alisema aliunda Kamati hiyo ambayo aliipa  jukumu la kusaidia kutafuta fedha za kuwalipa waamuzi ambao waligoma, lakini hakueleza kama ana mamlaka kikatiba kuunda Kamati.

Alisema baada ya kuundwa kwa Kamati hiyo ligi iliendelea kuchezwa kwa makubaliano ya deni litatafutiwa ufumbuzi wa haraka na waamuzi walikubali

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.