Kaimu
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Wilson Nkhambaku(kushoto) akimkabidhi Seni
Konda kitita cha shilingi milioni moja ikiwa ni zawadi baada ya kuibuka
mshindi katika mashinmdano ya Baiskeli Kanda ya Ziwa yaliyozaminiwa na
Kampuni ya Bia Tanzania kupitia kinywaji chake cha Safari Lager wakati
wa sherehe za maadhimisho ya siku Kuu ya Wakulima ya Nane nane.Kulia ni
Ofisa mauzo wa Kanda ya Ziwa, Malaki Sitaki.
Kaimu
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Wilson Nkhambaku(kushoto) akimkabidhi
Elizabeth Clement kitita cha shilingi laki saba ikiwa ni zawadi baada ya
kuibuka mshindi katika mashinmdano ya Baiskeli Kanda ya Ziwa
yaliyozaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania kupitia kinywaji chake cha
Safari Lager wakati wa sherehe za maadhimisho ya siku Kuu ya Wakulima ya
Nane nane.Kulia ni Ofisa mauzo wa Kanda ya Ziwa, Malaki Sitaki.
Washiriki
wa mashindano ya mbio za Baiskeli wakishindana wakati wakimaliza mbio
hizo katika uwanja wa mpira wa Kambarage mjini Shinyanga.
Mmoja ya washiriki wa mashindano ya mbio za baiskeli wanawake akimalizia mbio za kilometa 150.
Baadhi ya Baiskeli za wakazi wa Kanda ya ziwa wakiwa wamezipaki mara baada ya mashindano hayo wakimsikiliza mgeni rasmi
MKAZI
wa Manispaa ya Shinyanga Seni Konda, ameibuka bingwa upande wa
Wanaumena na kuzawadiwa kitita cha Shilingi Milioni moja katika
mashindano ya Mbio za Baiskeli Kanda ya Ziwa za Kilometa 220 kutoka
Shinyanga mpaka Wilayani Kahama na kurudi Shinyanga zilizofanyika
Mkoani Shinyanga wakati wa kusherehekea Siku Kuu ya Wakulima ya
Nanenane kwa udhamini wa Kampuni ya Bia Tanzania kupitia Bia yake ya
Safari Lager.
Katika
mashindano hayo yaliyoshirikisha washiriki zaidi ya 200 kutoka mikoa ya
Kanda ya Ziwa na Magharibi mshindi wa pili alikuwa ni Leonard Ng’wigulu
pia kutoka manispaa ambaye pia alijinyakulia zawadi ya shilingi 800,000
ambapo mshindi wa tatu Charles Makhirikhiri kutoka Shinyanga vijijini
alijinyakulia kitita sha shilingi 600,000.
Mshindi
wanne Charles clement alipata zawadi ya shilingi 500,000 ambapo wa tano
Nyanda Duba alijinyakulia shilingi 300,000 na mshindi wa sita hadi wa
kumi walipatiwa kifuta jasho cha shilingi 100,000 kila mmoja.
Kwa
upande wa washiriki wanawake waliokimbia umbali wa kilometa 150 kutoka
Shinyanga mjini hadi Isaka na kurejea tena Shinyanga mjini, Elizabeth
Clement aliibuka mshindi wa kwanza na kupata zawadi ya shilingi 700,000
ambapo mshindi wa pili Salome Donald alipata shilingi 500,000 na mshindi
wa tatu Berth Donald alijinyakulia shilingi 300,000.
Mshindi
wa nne kwa upande wa wanawake alikuwa ni Nyazobe Masanja aliyepata
shilingi 200,000 na mshindi wa tano Rabi Ng’wandu aliyejinyakulia
shilingi 150,000 ambapo pia kwa mshindi wa sita hadi wa kumi kila mmoja
alijipatia shilingi 100,000 kama kifuta jasho.
Mashindano
hayo pia yalihusisha mbio za walemavu waliotumia baiskeli za matairi
matatu ambapo walizunguka uwanja wa mpira wa Kambarage mizunguko 30
ambapo alikuwa ni Makande Ndelela kutoka manispaa aliyepata shilingi
100,000, mshindi wa pili Petro Thomas, shilingi 80,000 na watatu Ngalu
Ngamba aliyejinyakulia shilingi 60,000.
Akikabidhi
zawadi kwa washindi wa mbio hizo ambazo zimedhaminiwa na Kampuni ya Bia
Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager, mgeni rasmi Wilson
Nkhambaku ambaye ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga aliwapongeza
washiriki wote walioshiriki katika mashindano hayo.
Nkhambaku
alisema michezo ni moja ya sera za chama tawala CCM, lakini pia mbali
ya kuwa ni burudani lakini hutoa ajira kwa vijana wanaoshiriki michezo
hiyo.
Aidha
aliipongeza kampuni ya bia (TBL) ambapo aliwataka kuendelea na moyo huo
na kuiomba kufikiria uwezekano wa kuongeza viwango vya zawadi kwa
washiriki na kwamba ni vizuri mwakani kampuni ikatoa zawadi kwa
washiriki wote watakaojitokeza kushiriki mashindano hayo kwa viwango
tofauti ili mradi kila mshiriki aweze kujipatia chochote na kwamba
kitendo hicho kitawapa moyo wa kushiriki vijana wengi.
“Nakupongezeni
sana kwa moyo wenu wa kuwadhamini mashindano haya ya mbio za baiskeli
ikiwa leo hii ni mwaka wenu wa 15, hongereni sana, lakini niwaombe kitu
kimoja ni vizuri sasa mwakani mkaangalia uwezekano wa kuongeza viwango
vya zawadi ili iwe kivutio cha washiriki wengi kushiriki,” alisema
Nkhambaku.
Kwa
upande meneja mauzo kanda ya Ziwa wa kampuni ya Bia Tanzania (TBL)
Malaki Staki alisema kampuni yake imekuwa ikidhamini mashindano ya mbio
za baiskeli kwa mikoa ya kanda ya ziwa kwa lengo kukuza mchezo huo ambao
unapendwa na wakazi wengi wa mikoa ya kanda ya ziwa.
Staki
alisema mbali ya kukuza mchezo huo wa mbio za baiskeli lakini pia
umelenga kuwapatia kipato vijana wa kike na wa kiume wanaojitokeza
kushiriki mashindano hayo.
“Kwa
mwaka huu kampuni yetu imetumia kiasi cha shilingi milioni 5.9 kwa
ajili ya zawadi mbalimbali kwa washiriki tofauti na mwaka jana ambapo
tulitumia shilingi milioni 2.5, lakini pia mchezo huu ni moja ya
burudani kubwa kwa wakazi wa mikoa ya kanda ya ziwa, ambao sasa
tunawaomba waendelee kutumia bia yetu ya safari kwa wingi ili tuendelee
kudhamini mchezo huu,” alisema.
source; MICHUZI





0 comments:
Post a Comment