zanzibar

WAPEMBA WAPINGA UTEUZI WA BAUSI

Kocha Salum Baus wa Zanzibar Heroes ametaja kikosi kitakacho shiriki michuano ya Chaleng mwaka huu mjini Nairobi, akiwaacha manahodha wa timu hiyo Nadir Haroub 'Cannavaro' na Agrey Morris.

Katika kikosi hicho kilichotangazwa hapo jana na kudaiwa na baadhi ya wadau wa mpira wa miguu kutoka visiwani Pemba kuwa ni kikosi cha kombaini ya Ungaja si kikosi cha taifa ya Zanzibar inayounganisha visiwa vya Pemba na Unguja, hakujumuishwa kiungo mpya wa KMKM aliyetokea Azam FC Abdi Kassim 'Babi'..

Wanaopinga uteuzi wa BAusi wanasema kuwa, uteuzi wa kikosi cha Zanzibar hakikufuata makubaliano yaliyo wafikiana hapo awali ambapo kikosi cha Zanzibar herose kita teuliwa baada ya mchezo wa kombaini ya Pemba na Unguja.

Chanzo chetu cha habari kinaeleza kuwa, kikosi cha Zanzibar kitaundwa kutokana na wachezaji wa kombain ya Pemba na Unguja baada ya kufanyika mchezo huo, kinyume na ilivyo fanyika hivi sasa.

Wachezaji walioitwa kuunda kikosi cha Zanzibar heroes na kocha Salum Bausi na timu zao kwenye mabano ni walinda milango Mwadini Ali Mwadini (Azam fc), Abdallah Rashid ‘Babu’ (Ruvu Shooting) na Ali Suleiman Abdi (KMKM).

Walinzi ni Mohammed Azan ‘Brown’ (Polisi - Zanzibar), Waziri Salum (Azam ), Shafii Hassan (Malindi), Mohammed Faki (Zimamoto), Salum Haji Juma (Miembeni), Said Yussuf (Mtende Rangers), Mohammed Othman Mmanga (Jamhuri), Mussa Said Magarawa (Chwaka Stars) na Nassor Masoud ‘Cholo’ (Simba).

Viungo ni pamoja na Abdulhalim Humuod (Simba), Sabri Ali Makame (Oljoro JKT), Adeyoum Saleh (Simba) na Is-haka Othman (JKU), Ali Kani Mkanga (JKT Ruvu), Hamadi Mshamata (Chuoni), Hamadi Juma Issa na Masoud Ali Mohammed (Mtibwa Sugar).

Washambuliaji ni Seif Abdalla Rashid na Khamis Mcha Khamis ‘Viali’ wa Azam, Suleiman Kassim Suleiman ‘Solembe’ (Coastal Union), Amour Omar Mohammed ‘Janja’ (Miembeni) na Amir Omar Hamad (Oljoro JKT), Jaku Joma Jaku (Mafunzo), Faki Nahoda (Kimbunga F. C), Hassan Seif Ali (Mtibwa) na mfungaji bora wa mashindano ya kombe copa cola yaliyomalizika hivi karibuni Juma Ali Yussuf anaechezea timu ya New Vission inayoshiriki ligi daraja la central wilaya ya Mjini, Unguja.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.