simba

PHIRI APEWA MICHEZO MITATU, KISIGA ASIMAMISHWA


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhyJ7LvdFOVrWmHoxMlaWUtwXPCRc8laOrSVp7p9ESKSenZPZKuIzhJ08Nvjonasho9qRRBXiKbBufRkYXnbsxHRNV5VIPOxsk1W6_ubii1bHFz49sEqyAEuTrh5UBSEDaQd6blaIbMivYj/s1600/Phiri+1.JPG

Simba SC imetoa michezo mitatu kwa benchi la ufundi ambapo wanatakiwa kuambulia point kuanzia 7 mpaka 9 katikia michezo hiyo la sivyo benchi lote la ufundi litavunjwa.

Uwamuzi huo wa kutoa michezo mitatu inakuja baada ya Simba SC kukusanya pointi 5 katika michezo mitano na kufunga magoli 5 na kufungwa goli 5, ambapo imewaweka katika nafasi ya 10 katika msimamo wa ligi kuu ya vodacom.

Michezo hiyo mitatu iliyopewa benchi la ufundi la Simba SC linalo ongozwa na Patrick Phiri, ni mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar utakaochezwa katika uwanja Jamhuri wikiendi ijayo, na kisha kurejea Taifa na kuwakabili Ruvu shooting november 9 na mchezo wa tatu ni dhidi ya Kagera Sugar hapo desember 26 mwaka huu.

Kwa mujibu wa taarifa tulizo izpata toka katika kikao cha Simba SC kilichofanyika hii leo huko Mbeya ikiwa ni baada ya kutoka sare ya kufungana goli 1-1 na Tanzania Prisons, zinaeleza pia wachezaji watatu wa Simba SC wamesimamishwa kutokana na matokeo ya Sare kwa Simba SC katika michezo hiyo mitano.
Wachezji watatu waliozimamishwa ni pamoja na Amri Kiemba, Haruna Chanongo na Shaban Kisiga ambaye ameifungia Simba SC magoli mawili kati ya matano waliyo funga Simba SC.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.