Na Ally Mohammed, Zanzibar.
Matokeo mabovu ya Super falcon kumeanza kuwapa wasiwasi wadau wa soka visiwani Zanzibar na mashaka juu ya ushiriki wa timu hiyo katika ligi
klabu bingwa Afrika.
Super Falcon inayo iwakilisha Zanzibar katika ligi ya mabingwa Afrika imecheza michezo saba ambapo michezo yote amefungwa.
Katika michezo hiyo 7, mitatu ni michezo ya hatua ya makundi katika michuano ya Super8 BancABC. Ikiwa ni kabla ya kufungwa 3-1 na Jamhuri katika mechi ya kuwania ngao ya jamii.
Super Falcon walipoteza kwa Coastal union goli 2-0 katika mchezo wa kujiandaa na ligi kuu ya Zanzibar Grand Malt.
Super Falcon mpaka sasa wamecheza michezo miwili ya ligi ambapo wamepoteza yote kwa kufungwa 2-0 katika mchezo wa kwanza kabla ya leo kufungwa 2-1.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment