VPL

YANGA YAKAMATWA, SIMBA NYAVU NYEUPE, AZAM YAKATA MWIKO

Michezo ya ligi kuu ya Vodacom imeanza leo katika viwanja 7 vya mikoa 6, ambapo Azam FC, Simba SC, Coastal na JKT Ruvu wakiibuka na ushindi wakati Yanga wakilazimishwa sare na wanajelajela Prisons.


KULIA NGASSA, KUSHOTO OKWI, KATI AKUFO

Msemo wa kulia Ngassa kushoto Okwi kati Akufo kule Boban ulitawala sana katika vichwa vya mashabiki wa Simba SC, ambapo leo wameuwanza vyema msimu baada ya kila mshambuliaji kutoka na goli lake hii leo.

Simba SC waliwakabili African lyon ya Mbagala katika uwanja wa Taifa na kufanikiwa kuwachapa Lyon goli 3-0, ikiwa ni clean shiti ya kwanza baada ya kufanya hivyo katika michuano ya Kagame Cup.

Alikuwa Emanuel Okwi katika dakika ya 33 kuwanyanyuwa mashabiki wa Simba SC, kabla ya kukaa kimya pale Mwinyi Kazimoto alipo ushika mpira katika eneo la hatari na mwamuzi kuamuru kupigwa penati iliyopanguliwa na Juma Kaseja katika dakika 35.

Wakati Lyon wakishanga Mrisho Ngassa aliumalizia mpira wa Said Cholo katika dakika ya 36 na kuiandikia Simba goli la pili na kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa goli 2-0.

Katika dakika ya 57 Emanuel Okwi aliangushwa katika eneo la hatari na Daniel Akuffo akiifungia goli la 3 Simba SC kwa Mkwaju wa penati na kumaliza mchezo kwa simba kushinda goli 3-0.


AZAM WAPATA USHINDI KWA MARA YA KWANZA KAITABA
Kwa mara ya kwanza Azam FC leo wameondoka na point zote tatu katika uwanja wa Kaitaba baada ya kuichapa goli 1-0 Kagera Sugar.

Goli hilo pekee la Azam FC lilifungwa na Abdulhalim Homoud katika dakika ya 57, katika mchezo uliokuwa wa pande zote mbili.


SAFU KALI YA USHAMBULIAJI YATOKA KAPA SOKOINE

Safu ya ushambuliaji ya Yanga iliyo onyesha makali katika michuano ya Kagame na michezo ya kirafiki leo wameshindwa kuziona nyavu za Prisons ya Mbeya.


COASTAL YAAMKIA KWA MGAMBO

Baada ya kufanya vibaya katika michezo ya kirafiki, Coastal Union imeanza vyema ligi kuu baada ya kuwachapa goli 1-0 wageni wa ligi kuu Mgambo JKT.

Goli la coastal limefungwa na Jerry Santo katika kipindi cha pili.


MATOKEO MENGINE

COASTAL UNION 1-0 MGAMBO SHOOTING

PRISONS 0-0 YANGA

AZAM FC 1-0 KAGERA SUGAR

SIMBA SC 3-0 AFRICAN LYON

POLISI MORO 0-0 MTIBWA SUGAR

JKT RUVU 2-1 RUVU SHOOTING

TOTO AFRICAN 1-1 JKT OLJORO

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.