mtazamo

Yanga walimrahisishia kazi Nkongo



Habari za kazi wapendwa wasomaji na wafuatiliaji wa kazi za Aboodmsuni, leo narejea katika tukio lililo tokea mwishoni mwa juma lililo pita katika mchezo kati ya Yanga na Azam FC.

Baada ya mchezo huo uliotawaliwa na vurugu, mengi yalisemwa na mwisho wa siku wachezaji walio husishwa na vurugu hizo wametiwa pingu la kutocheza soka kwa vipindi tofauti.

Madai ya vurugu hizo ni madai ya kwamba mwamuzi Israel Nkongo alipewa fedha na Azam FC. Na kama tetesi hizo zilikuwa na ukweli ndani yake basi Yanga walimrahisishia Kazi Nkongo katika kufikia dhamira yake kwa sababu zifuatazo:

1. MADHAMBI KATIKA ENEO LA HATARI

Dakika za mwanzo wa mchezo Athuman Iddi Chuji alimfanyia madhambi mchezaji wa Azam katika eneo la hatari, wakati waki okoa mpira wa kona. Faulo hiyo ingezaa penati ya mapema na kuwapa goli la kuongoza Azam na mwamuzi kutimiza dhamira yake.

Lakini mwamuzi alipotezea hiyo na kuuwacha mpira uwendelea ambapo hakukawia Azam wakapata goli la kuongoza. Kwa kitendo cha Chuji kucheza madhambi katika eneo la hatari, tena isiyokuwa ya msingi, ingetimiza dhamira ya Nkongo mapema.

2. KADI ZA NJANO

Katika mchezo huo Yanga walipata baadhi ya kadi za njano za kujitakia, madhalani kadi ya kwanza ya Niyonzima, ilikuwa ya kujitakia na tena kama mnadhana ya mwamuzi yupo upande wa wapinzani wenu.

Kulikuwa hakuna haja ya Niyonzima kumtengenezea mazingira Nkongo kumpatia kadi ya kwanza ya njano katika mchezo muhimu kama ule.

3. MIPANGO NNJE YA UWANJA

Hapa nazungumzia kitu kilichokuwa na kinaendelea kumfanya Morinho kuwa juu na kitu hicho kinaitwa 'Mind game'. Kwetu tumezoe kuziita Fitna za mpira ambapo kwa waswahili hulengwa katika kuwahonga wachezaji wa timu pinzani, na mwamuzi vile vile kwenda kwa waganga.

Katika mchezo huo fitna zilipikwa na mashabiki na baadhi ya vyombo vya habari ambavyo vilizungumzia kuhongwa kwa mwamuzi kabla ya mchezo na kuwaingia wachezaji wa yanga na kuamini mwamuzi yupo upande wa wapinzani hata kabla mchezo haujaanza na pale maamuzi yaliyokuwa yanafanywa juu yao waliamini wanaonewa.

Hali hiyo ilikuwa mbaya zaidi pale Azam walipo pata goli la kuongoza dakika ya 5 ya mchezo. Na kuashiria kuwa mchezo huo kutomalizika bila ya fujo.

Viongozi wa Yanga walishindwa kuwaanda wachezaji wake namna ya kukabiliana na hayo yanayosemwa kama yana ukweli ndani yake, ama kupinga mwamuzi kuchezesha mpambano huo, na taarifa zinadai kuwa uongozi waliwaambia baadhi ya wachezaji ya kwamba Mwamuzi atakuwa upande wa timu pinzani (Azam FC) wakisahau kuwapa maelekezo ya kuto mpa nafasi mwamuzi kutoa maamuzi yatakayo igharimu timu. Na hilo suala halikuwa la kuwaambia wachezaji wachache.


Na hitimisha Kwa kile kilichotokea jumamosi ya machi 10 nimeelewa ni namna gani timu zetu zinavyoshindwa kupata matokeo wakiwa ugenini hususan pale wanapocheza na timu zenye asili ya kiarabu.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.