Akizungumza mapema leo Dr Kaseko amesema Mlawa hakuvujika mguu kama ambavyo taarifa zilizotolewa awali kupitia vyombo mablimbali vya habari isipokuwa mshambuliji huyo alipata mshituko mdogo kwenye kifundo cha mkuu wa kulia.
“Mlawa hakuvunjika mguu kama taarifa za mwanzo lizivyotolewa kilichotekea ni kwamba alipata mshituko kwenye kifundo cha mguu baada ya kipa wa JKT Ruvu kumkanyaga wakati akijiandaa kupiga mpira, kilichomsaidia kutokuvunjika mguu ni kwa sababu alikuwa kwenye mwendo wa kasi, tumemfanyia matibabu ya haraka na tayari yuko kwenye hali nzuri, imani yangu kuwa atakuwa sehemu ya kikosi kwenye mchezo wetu ujao dhidi ya Prison” alisema Dr Kaseko.
Geofrey Mlawa amejiunga na City msimu huu akitokea Kimondo Fc ya Mbozi jijini Mbeya na tayari amekuwa mchezaji muhimu kwenye safu ya ushambuliaji.
CHANZO: mbeyacityfc.com
0 comments:
Post a Comment