VPL

LYON WAIKOMALIA YANGA, WATOA SARE

Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya vodacom Yanga SC leo wamelazimishwa sare na African Lyon, katika mchezo wa ligi kuu ya vodacom uliochezwa katiuka uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.

Katika mchezo huo wa leo ulishihudia mchezo ukienda mapumziko wakiwa sare ya bila  kufungana huku African lyon wakitumia muda mwingi kujilinda na kupelekea yanga kushindwa kutengeneza nafasi yoyote ya goli.

Kipindi cha  piloi African Lyon walianza kwa kupeleka mashambulizi na katika dakika ya 59 walifanikiwa kuandika goli la kuongiza kupitia kwa Ludovic.

Kuingia kwa goli hilo kulipelekea Yanga SC kuongeza nguvu katika eneo lao la ushambuliaji kwa kumuingiza Chirwa akichukuwa nafasi ya Kamusoko na Martins akichukuwa nafasi ya Kaseke.

Katika dakika ya 74 Amisi Tambwe aliisawazishia Yanga SC na kupelekea mchezo kumalizika kwa sare ya goli 1-1. 

About dada

0 comments:

Powered by Blogger.