CECAFA

DKT. SHEIN 'ATOA NDEGE' KUIREJESHA ZANZIBAR HEROES

Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein amesema timu ya taifa ya Zanzibar, ‘Zanzibar Heroes’ itarejea visiwani humo kwa ndege badala ya njia nyingine ilizotumia wakati ikielekea nchini Kenya kwaajili ya michuano ya kombe la CECAFA.

Dkt. Shein amesema kwa hatua ambayo Zanzibar Heroes imefikia wao kama serikali wanalazimika kuthamini jitihada za vijana hao huku akiahidi donge nono la zawadi ambalo litawekwa wazi pindi timu hiyo itakaporejea.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwenye ofisi za wizara ya michezo ya Zanzibar zilizopo eneo la Kikwajuni mjini Unguja, waziri mwenye dhamana na michezo Rashid Ally Juma, ndiye aliyewasilisha salamu hizo za Dkt. Shein.

Zanzibar Heroes inashuka dimbani kesho kuvaana na wenyeji Kenya katika mchezo wa fainali ya michuano hiyo utakaorushwa mbashara na Azam TV.

About dada

0 comments:

Powered by Blogger.