TFF

TFF:Nkongo alikuwa sahihi

Kalunde Jamal

KAMATI ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyokutana Jijini Dar es Salaam, imesema mwamuzi aliyechezesha mechi ya Yanga na Azam, Israel Nkongo hakuwa na makosa.

Mchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa mwishoni mwa wiki ulitawaliwa na vurugu toka wachezaji wa Yanga, ambao baadhi walimshambulia mwamuzi Israel Nkongo.

Afisa Habari wa TFF, Boniface Wambura alisema, Kamati ya Ligi haijabaini kosa lolote kufanywa na mwamuzi na kwamba alikuwa sahihi sehemu kubwa ya mchezo.

Wambura alisema kuwa, taarifa kwamba mchezo ulimshinda mwamuzi kama inavyodaiwa, siyo sahihi ndiyo maana aliweza kuchezesha mchezo mpaka mwisho pamoja na kupigwa.

Alisema kuna kanuni ambayo inamlinda mwamuzi kusimamisha pambano anapopata misukosuko ikiwemo kupigwa, lakini kwa kuonyesha alikuwa makini na kazi yake hakuitumia na alimudu kumaliza pambano kitu ambacho ni ngumu.

"Kamati imetoa tamko mwamuzi alikuwa sahihi baada ya kupitia taarifa ya kamisaa na ya mwamuzi mwenyewe imeonekana hakuwa na kosa na mchezo aliumudu," alisema Wambura.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.