yanga

MSUVA APIGA GOLI LAKE LA KWANZA YANGA

Simon Msuva, kwa msaada wa Bin Zubeiry
Mshabuliaji chipukizi wa Yanga aliyesajiliwa toka Moro United Happygod Simon Msuva amefunga goli lake la kwanza akiwa na uzi wa Yanga katika ushindi wa goli 4-0 walio upata mbele ya African Lyon.

Mchezo huo wa kirafiki ulichezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, na kushuhudia Yanga wakiandika goli la kwanza katika dakika ya 6 kupitia kwa mshambuliaji wao mpya waliye msajili toka Atletico ya Burundi, Didier Kavumbangu na goli hilo likiwapeleka Yanga mapumziko wakiwa mbele kwa goli moja.

Katika kipindi cha pili Yanga waliingia katika nyavu za African Lyon mara tatu, ambapo Haruna Niyonzima ndiye aliyekuwa wa mwanzo kutikisa nyavu za Lyon kwa mkwaju wa penati baada ya Msuva kukatuliwa na Semmy Kessi katika eneo la hatari katika dakika ya 56.

Msuva aliifungia Yanga goli la tatu katika dakika ya 72 baada ya kupokea pasi ya kiungo chipukizi Franky Domayo aliyeingia kuchukuwa nafasi ya Athuman Iddi Chuji kabla ya Jerry Tegete kuhitimasha karamu ya magoli katika dakika za nyongeza.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.