basketball

KIKAPU YATAKA mil100

Imani Makongoro

SHIRIKISHO la Mpira wa Kikapu Tanzania, TBF, linahitaji Sh100 milioni kufanikisha michuano ya Kombe la Taifa iliyopangwa kufanyika mapema Oktoba mkoani Tanga.

Rais wa TBF, Mussa Mziya aliliambia gazeti hili kwamba fedha hizo ni za gharama ya chakula, malazi, huduma muhimu wakati wote wa michuano na usafiri wa ndani kwa wachezaji wote watakaoshiriki michuano hiyo.

Kwa mujibu wa Mziya alisema kwa sasa hawana fedha yoyote licha ya kuhangaika huku na kule kutafuta wafadhili kufanikisha michuano hiyo yenye lengo la kuandaa timu kwa ajili ya mashindano mbalimbali ya kimataifa ikiwemo yale ya kanda ya tano yatakayofanyika Desemba jijini Dar es Salaam.

"Tukifanikiwa kupata ufadhili tutawagharamia wachezaji wote, tukikosa kila mkoa utalazimika kuwagharamia wachezaji wake," alisema Mziya.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.