basketball

EASTERN ZONE YANGARA

TIMU ya Eastern Zone One imeanza vyema mashindano ya mpira wa kikapu ya Sprite BBall Kitaa kwa kuifunga Eastern Zone Two 34 -15 katika mchezo ulichezwa kwenye uwanja wa Spider Gymkhana Club jijini Dar es Salaam juzi.

Ikishangiliwa na mashabiki wake, timu hiyo ya Sinza jijini Dar es Salaam ilianza mchezo huo kwa kasi na kufanikiwa kupata pointi za mapema na kuzima kabisa ndoto za wapinzani wao kushinda mchezo huo.

Katika mchezo wa kwanza uliopigwa kwenye uwanja huo, timu ya Western Zone Three ilifanya kazi ya ziada kuwashinda Western Zone Four 40-37 katika mchezo uliokuwa wa kusisimua na wenye upinzani mkali.

Timu ya Western Zone Four inayoundwa na wachezaji kutoka Ilala Boma na Magomeni, ilianza mchezo huo kwa kusuasua na kuwawezesha wapinzani wao kuongoza kwa magoli sita katika dakika za mwazo kabla ya kuzinduka na kushika usukani na hatimaye kuibuka washindi katika mchezo huo Katika mchezo mwingine, timu ya Western One ilifanikiwa kushinda magoli 27-17 dhidi ya Western Two.

Washindi walitawala mchezo huo tangu mwanzo na kuonesha dalili mapema kuwa wangeibuka kidedea. Mashindano ya BBall Kitaa yenye lengo la kukuza vipaji vya wachezaji wa mpira wa kikapu yatakuwa yanafanyika kila Jumapili hadi Juni 29.

About Unknown

0 comments:

Powered by Blogger.