basketball

KIKAPU KIKATAA YAZIDI KUPAMBA

MASHINDANO ya Sprite Bball Kitaa yamezidi kupamba moto katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam mwishoni wa wiki ambapo timu nane za mchezo wa mpira wa kikapu zilichuana vikali.

Katika mchezo wa kwanza timu ya Western Zone One iliifunga timu ya Western Zone Two kwa pointi 39 kwa 30 katika mchezo uliokuwa na upinzani mkali.

Mchezo wa pili ulizikutanisha timu ya Eastern Zone Three na Eastern Zone Four mchezo huu ulimalizika kwa vijana wa timu ya Eastern Zote Four kuwabwaga wenzao wa Eastern Zone Three kwa pointi 42 kwa 32.

Katika mashinadano hayo yaliyokuwa ya kudunk na mitupo mitatu, katika mchezo wa tatu ulizikutanisha timu za Eastern Zote One ambayo iliifunga timu ya Eastern Zone Two kwa pointi 26 kwa 19.

About Unknown

0 comments:

Powered by Blogger.