basketball

NEW WEST HOI ZANZIBAR

TIMU za mpira wa kikapu za New West za miaka minane hadi 15 na miaka 15 hadi 20, zimeshindwa kutamba mbele ya timu za Stone Town kwa kukubali kichapo katika michezo yao waliyocheza kwa nyakati tofauti.

Timu hizo zinazoshiriki michuano ya vijana, zilishuka kucheza kwenye Uwanja wa Maisara, Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.

Saa tisa alasiri juzi ilishuka dimbani timu ya miaka 8 hadi 15 ambayo ilifungwa vikapu 32-29 katika mchezo ambao ulikuwa na ushindani wa hali ya juu.

Hata hivyo, New West inayoundwa na wachezaji kuanzia miaka 15 hadi 20 ilifungwa vikapu 30-29, huku mchezo huo ukionesha upinzani wa hali ya juu.

Itakumbukwa kuwa katika mechi zao za mwanzo, Stone Towne zilipoteza kwa timu zao mbili ambapo kubwa ilifungwa na Cavarius vikapu 35-22 na ya wadogo ikifungwa na timu hiyo hiyo vikapu 35-30.

About Unknown

0 comments:

Powered by Blogger.