basketball

TBF YAANDA MICHUANO YA WANAWAKE DAR

SHIRIKISHO la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), limeandaa mashindano ya wanawake yatakayoanza kutimua vumbi kuanzia Aprili 8 hadi 16, mwaka huu kwenye Uwanja wa Ndani wa Taifa, Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Kamishna wa Ufundi na Uendeshaji Mashindano wa TBF, Manase Zablon, mashindano hayo yatafunguliwa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk Fenella Mukangara.

Zablon alisema timu 16 tayari zimethibitisha kushiriki michuano hiyo ambazo ni Jeshi Stars, JKT Stars, Tanzania Prisons, Cargo Dar es Salaam, Vijana Queen, SMUT, Morogoro Warriors, Tanga Queen, Dodoma, Mbeya na Mwanza.

“Maandalizi yanakwenda vizuri tunategemea timu zitajitokeza zaidi kwa ajili ya michuano hiyo muhimu katika kujiweka katika nafasi nzuri ya kushiriki michuano ya taifa, mwaka huu,” alisema Zablon.

Alisema anategemea mashindano ya mwaka huu yatakuwa na upinzani mkali kutokana na kila timu kuonesha kujiandaa vizuri.

Alisema timu nyingine zinazotaka kushiriki zinatakiwa ziwe zimethibitisha ushiriki wao hadi kufika Aprili 4, mwaka huu, kwa ajili ya kuanza mchakato wa kupanga ratiba ya mashindano.

About Unknown

0 comments:

Powered by Blogger.