basketball

BBALL KITAA SHUGHULI NI LEO

PAMBANO la kukata na shoka la mpira wa kikapu la Bball Kitaa linafanyika leo jijini Dar es Salaam kwa kuzikutanisha timu mbili zenye upinzani wa hali ya juu.

Mashindano ya mwaka huu ya Bball Kitaa yamedhaminiwa na Sprite na pambano hilo la leo litazikutanisha timu za Kanda ya Mashariki 2, ambayo itakuwa na wachezaji kutoka Msasani, Oysterbay na Masaki dhidi ya wenzao wa Magharibi One inayoundwa na wachezaji kutoka Kanda ya Mbezi Beach, Kunduchi na Tegeta.

Mchezo huo unaotarajiwa kuvuta hisia za mashabiki wengi wa mchezo huo kutoka pande zote za jiji la Dar es Salaam, utafanyika katika katika eneo la Bball Kitaa Park, jirani na eneo maarufu la Dar es Salaam Gymkhana Club.

Lengo la mchezo huo ni kuwaweka tayari wadau wa mpira wa kikapu kabla ya mashindano makubwa ya Julai, ambapo mabingwa watetezi Kanda ya Magharibi 4 inayounda na wachezaji kutoka Temeke na Mbagala, Kanda ya Mashariki 1, Kanda ya Mashariki 3, Kanda ya Magharibi 2, Kanda ya Magharibi 3 na Kanda ya Magharibi 4.

Washindi wa mashindano yajayo ya Kanda watapewa zawadi ya fedha taslimu Sh milioni 5.


 
CHANZO: HABARI LEO

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.