basketball

8 KUSHIRIKI SUPER CUP

ZAIDI ya timu nane za kikapu mkoa wa Dar es Salaam zinatarajiwa kushiriki kwenye mashindano ya Super Cup yatakayoanza kutimua vumbi kuanzia keshokutwa.

Akizungumza na gazeti hili Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Kikapu Dar es Salam (DB), Mwenze Kabinda alisema mashindano hayo yatatoa mabingwa ambao watawakilisha mkoa kwenye michuano ya taifa itakayofanyika baadaye mwezi huu.

Alisema maandalizi kuelekea kwenye michuano hiyo yamekamilika na kwamba wanatarajia mashindano hayo yatapata upinzani mkali na kupata timu bora itakayofanya vizuri kitaifa.

“Tuna timu nane za wanaume ambazo zitashiriki lengo ni kuhakikisha tunapata timu ambazo zitaenda kutuwakilisha vyema kwenye mashindano ya kitaifa, tunategemea yatakuwa ni mazuri,” alisema.

Alitaja timu hizo kuwa ni JKT, Savio, Vijana, Mgulani, Jogoo, Magereza, Don Bosco Youngster na Pazi. Kabinda ameomba wadau mbalimbali kujitokeza na kuunga mkono mashindano hayo kwa ajili ya kupata fedha za kununua zawadi kwa washindi na wachezaji bora.

Chanzo: Habari Leo

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.