basketball

ZONGA ADAIWA KUTAFUNA mil 40/-

Katibu Mkuu wa TBF Saleh Zonga
KATIBU Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), Saleh Zonga amesema kuwa anashangazwa na taarifa kuwa amesimamishwa kwa kula dola 20,000 (zaidi ya Sh milioni 40) kwa ajili ya ujenzi wa viwanja vya mchezo huo.

Pia Zonga alisema leo atatoa ufafanuzi huku akisisitiza kuwa, fedha hizo yuko tayari kuziweka katika akaunti ya TBF.

Akizungumza na gazeti hili jana, Zonga alikiri kupokea fedha hizo ambazo ziliwekwa katika akaunti yake baada ya yeye kuziomba binafsi kwa wafadhili nje ya nchi.

Alisema kuwa anapinga kusimamishwa kwake kwa kuwa hakufuata taratibu, ambapo alisisitiza kuwa fedha hizo aliziomba yeye kama Zonga na ndio maana ziliingizwa katika akaunti yake.

Zonga alisema kuwa leo atatoa ufafanuzi wa fedha hizo na yuko tayari kuziweka katika akaunti ya shirikisho hilo. Alisema kuwa feha hizo zililetwa kwake ili kujenga viwanja vya mchezo huo kwa ajili ya maendeleo ya mchezo huo hapa nchini.

Alisema kuwa mwenyekiti wa TBF, Injinia John Bandie hana mamlaka ya kumsimamisha yeye kama katibu wa shirikisho hilo.

Bandie akizungumza na gazeti hili alisema kuwa Zonga alichukua fedha hizo kutoka katika akaunti ya shirikisho na kuzipeleka kusikojulikana.

Alisema bodi ya TBF itakutana hivi karibuni kutoa maamuzi ya kufanya kama atimuliwe kabisa na kuburuzwa katika vyombo vya kisheria au la.

Alisema kuwa fedha hizo ziliingia katika akaunti Septemba mwaka jana na wao waligundua mwishoni mwa mwaka uliopita.

Chanzo: Habari leo

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.