basketball

MAFUNZO YA KIKAPU KUFANYIKA IRINGA

KOCHA wa timu ya mpira wa Kikapu Matthew Mc Colister leo ataendesha mafunzo ya mchezo huo mkoani Iringa. Mafunzo hayo yanawalenga wachezaji chipukizi kwa ajili ya kuwaanda kushindana baadaye.

Colister yuko nchini kwa ajili ya kuinoa timu ya taifa ya kikapu, lakini pia anatumia fursa hiyo kuendesha mafunzo ya mchezo huo.

Akizungumza na gazeti hili jana, Kamishna wa Ufundi na Uendeshaji wa Mashindano wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), Manase Zabron alisema mkufunzi huyo atakuwa Iringa kwa siku mbili.

Alisema baada ya kumaliza kuendesha mafunzo hayo Iringa, atasafiri kwenda mkoani Dodoma kwa kazi hiyo.

"Baada ya kumaliza majukumu ya Dodoma, ataelekea Morogoro ambako pia ataendesha mafunzo na kurejea Dar es Salaam.

Alisema lengo lao ni kuona ndani ya wiki mbili atakuwa amekamilisha kazi hiyo kabla ya kuanza programu ya kuinoa timu ya taifa.

Matthew anatarajia kusaini mkataba wa mwaka mmoja kuinoa timu ya taifa, kwa mujibu wa TBF.

Chanzo: Nipashe

About Unknown

0 comments:

Powered by Blogger.