simba

USAJILI WA SIMBA SC


Klabu ya Simba inapenda kutangaza marekebisho madogo ya usajili iliyoyafanya kutokana na mapendekezo ya benchi la ufundi chini ya kocha Mkuu Joseph Omog.

Kwenye maboresho hayo klabu imewapandisha wachezaji wawili wa kikosi cha vijana, Beki Vicent Costa na nahodha wa kikosi hicho mshambuliaji Moses Kitandu

Sambamba na hao, klabu imewapeleka kwa mkopo Awadh Juma na Malika Ndeule kwenye Timu ya Mwadui Fc ya Shinyanga, pamoja na Emmanuel Semwanza atakaekwenda Maji Maji Fc ya Songea,

Huku pia klabu ikiachana rasmi na Golikipa mua-Ivory Coast Vicent Agban na kiungo kutoka Kongo Mussa Ndusha.

Sambamba na kuwasajili wachezaji raia wa Ghana, kipa Daniel Agyei na kiungo James Kotei, huku tukikamilisha taratibu za usajili kwa washambuliaji Pastory Athanas kutoka Stand United na Juma Luizio anayekuja kwa mkopo toka Zesco ya Zambia.

Halikadhalika klabu imemrejesha Ame Alli kwenye timu yake ya Azam ambayo ilimleta kwetu kwa mkopo.

Tunaamini maboresho haya yataongeza chachu ya ushindani katik kikosi chetu na Hatimaye kutupa mataji msimu huu.

Niwaarifu pia timu yetu imeondoka asubuhi hii kuelekea Mtwara kwa ajili ya mchezo wetu wa kwanza mzunguko wa pili dhidi ya Ndanda Fc, mchezo utakaopigwa siku ya jumapili ya tarehe 18/12/2016 huko Mtwara.

Imetolewa na ;
Haji S. Manara
Mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa Simba Sc
SIMBA NGUVU MOJA


KIKOSI CHA SIMBA SC

MAKIPA : Daniel Agyei, Dennis Richard, Peter Manyika

MABEKI : Mohamed Hussein, Abdi Banda, Hamad Juma, Janvier Bokungu, Method Mwanjali, Juuko Murshid, Novatus Lufunga, Vicent Costa

VIUNGO : Said Ndemla, Muzammil Yassin, Jonas Mkude, James Kotei, Mohamed Ibrahim, Mwinyi Kazimoto

MAWINGA : Shiza Kichuya, Jamal Mnyate, Hija Ugando

WASHAMBULIAJI :Ibrahim Ajibu, Juma Luizo, Frederic Blagnon, Laudit Mavugo, Pastory Athanas, Moses Kitandu

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.