Kikosi Cha Zanziba Heroes cha tajwa

Siku moja baada ya kuteuliwa na Kamati Tendaji ya Zfa Taifa kuwa Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes ambayo itashiriki michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge, baadaye mwezi huu mjini Kampala, Uganda, Salum Bausi Nassor ametangaza majina ya wachezaji 26, watakaoanza mazoezi kuanzia Jumanne ijayo.

Akitangaza majina ya wachezaji hao mbele ya waandishi wa habari katika ukumbi wa Zanzibar Ocean View, Salum Bausi, amesema licha ya muda mfupi alionao kuandaa kikosi cha ushindani katika mashindano hayo, lakini amezingati mambo muhimu katika uteuzi huo, huku akisema uteuzi huo haukuingiliwa na viongozi wa chama cha mpira wa miguu visiwani Zanzibar na kusisitiza suala la nidhamu ndio kigezo cha msingi katika uteuzi huo.

Amewataja waliochaguliwa katika kikosi cha Zanzibar Heroes kuwa ni:-

Walinda mlango ni; Mwadini Ali (Azam), Suleiman Hamad (Black Sella), Abdalla Juma (Kipanga).

Walinzi; Nassor Masoud 'Cholo' (Simba), Salmin Haji Nuhu (Azam), Agrey Moris (Azam), Nadir Haroub Ali 'Canavaro' (Yanga), Aziz Said Ali (Kmkm), Mohammed Juma Azan (JKU), Ali Mohammed Seif (Mtende Rangers).

Viungo; Hamad Mshamata (Chuoni), Ali Bakar (Mtende Rangers), Is-haka Mohammed (JKU), Twaha Mohammed(Mtibwa Sugar), Suleiman Kassim 'Selembe' (Coastal Union), Saad Ali Makame (Zanzibar All Stars), Makame Gozi (Zimamoto), Issa Othman Ali (Miembeni), Aleyuu Saleh (Black Sella), Abdulhalim Humoud (Azam), Khamis Mcha Khamis 'Viali' (Azam).

Washambuliaji; Amir Hamad (JKT Oljoro), Jaku Joma Jaku (Mafunzo), Abdallah Othman (Jamhuri), Nassor Juma (JKU), Faki Mwalim (Chipukizi).

Wachezaji hao wanatarajiwa kuchujwa wiki ya mwisho kabla ya mashindano na kubakia wachezaji 20 ambao wanatarajia kuingia kambini kujiandaa na safari ya kuelekea Kampala, Uganda tayari kwa michuano ya Chalenji.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.