VPL

YANGA AZAM NGUVU SAWA


Ligi Kuu Tanzania bara imeendelea Jumamosi hii huku Mechi Kati ya vinara wa Ligi Yanga na Azam imeshuhudiwa kuishia sare mabao 2-2 Katika mchezo ulichezwa kwenye Uwanja wa Taifa.

Azam walikuwa wa kwanza Kuwa mbele ya Yanga Kwa bao 1-0 alilojifunga beki Juma Abdul kwenye Dakika ya 10 kabla ya mchezaji huyo huyo kurekebisha makosa yake Na kupachika bao la kusawazisha Kwa Yanga kwenye Dakika ya 28.

Yanga waliendelea kuonyesha moto wao na wakajipatia bao Lao lapili kupitia mshambuliaji wao mahiri Donald Ngoma kwenye Dakika 42, na hadi mapumzikoni Yanga iliongoza kwa mabao 2-1 dhidi ya Azam.

Azam haikutaka kubaki nyuma na jitihada zao zikazaa matunda pale Nahodha wa timu Hio mshambuliaji John Bocc alipofunga bao la kusawazisha kwenye Dakika ya 70 na kulazimisha sare ya mabao 2-2 Kati ya Pande hizo mbili.

Matokeo mengine ya mechi Za Ligi Kuu Tanzania bara jumamosi Hii:
Kagera Sugar 1-1 Mgambo Shooting
Tanzania Prisons 1-0 Stand United
JKT Ruvu 1-0 Mwadui
Mtibwa Sugar 3-0 Coastal Union
African Sports 0-0 Majimaji
Toto Africans 0-0 Ndanda

About dada

0 comments:

Powered by Blogger.