vilabu

MANDAWA ATUWA MTIBWA, WAKIANZA MAZOEZI LEO

Timu ya Mtibwa Sugar inaanza rasmi mazoezi siku ya Jumatatu tarehe 11/07/2016 kujiandaa na msimu wa ligi wa 2016/17. Mazoezi yataanzia jijini Dar kwa wiki moja na baada ya hapo timu itaelekea kambini Mtibwa.

Katika mazoezi ya Mtibwa kutakuwa na sura kadhaa mpya wakiwemo mshambuliaji Rashid Mandawa ambaye amesajiliwa kutoka klabu ya Mwadui ya Shinyanga na beki wa kati Kassian Ponera ambaye msimu uliopita alichezea timu ya Ndanda ya Mtwara. Aidha katika usajili wetu, tumefanikiwa kuwaongezea mikataba wachezaji wetu kadhaa wakiwemo golikipa Said Mohamed na beki wa kati Salim Mbonde ambao walimaliza mikataba yao na walikuwa wakiwaniwa na timu mbalimbali.

Usajili unaendelea kwa umakini mkubwa chini ya Mwalimu Mayanga kuziba mapengo hususan kwenye eneo la kiungo ambako tumeondokewa na Mzamiru Yassin, Mohamed Ibrahim na Shiza Kichuya ambao wote wameenda Simba.

Chanzo: www.mtibwasugar.co.tz/

About dada

0 comments:

Powered by Blogger.