ZGPL

ZFA YAWAOMBA GRAND MALT KUENDELEA KUDHAMINI LIGI


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhPUP_TY6rf0eh23-pATqE8IWcpcOuQx_ERnTOk1c0gn8tyGztdlxr1fd39IJJjoqdnYbpAn2aF-Lc9BniCd_ijsGpYsCF6qf1cuQv2t8quY4FrNtVQc6JMHlRpoJ2loos4k8UBu8nLdkc/s1600/Zanzibar-Football-Association2.jpg

CHAMA cha Soka Zanzibar (ZFA), kimesema kuwa kimeshatuma maombi kwa mdhamini mkuu wa Ligi Kuu ya Zanzibar, Grand Malt kumwomba adhamini tena ligi hiyo baada ya kumaliza mkataba wake wa miaka mitatu.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Ufundi wa chama hicho, Masoud Attai alipozungumza na waandishi wa habari huko ofisini kwao Amaan mjini hapa.

Attai alisema pamoja na kuwa mdhamini huyo tayari anamaliza muda wake wa udhamini msimu huu, lakini uongozi wameshaanza kupeleka maombi yao ili asajili tena kwa kipindi kingine cha miaka mitatu.

“Kiukweli kwamba mdhamini amefika miaka yake mitatu, lakini ni kwamba bado tunaendelea kuwasiliana naye na tumeshaanza kupeleka maombi yetu kutaka adhamini tena,” alisema.

Hata hivyo, alisema kwa bahati nzuri mpaka sasa hawajajibiwa kwamba ombi hilo amelikubali au la, lakini kama waungwana ana imani kuwa wanatarajia wataendelea nao.

“Tumeshawapelekea hilo ombi letu na wametuambia kuwa tutakutana ili tulijadili hilo suala, kwa hivyo hatukuwa na nia kwamba watafute mdhamini mwingine wakati yule ambaye tunaendelea naye na bado anafanya vizuri tunampa nafasi tena mpaka pale atakaposema kuwa sitoendelea,” alisema.

Attai alipoulizwa ni siku gani wanatarajia kukutana, alisema suala la wao wadhamini kuwapa nafasi ya kukutana kwani wao kubwa walilolifanya ni kupeleka maombi yao ambayo walisema watakaa na kuifanyia kazi pamoja na Bodi yake halafu tena baadaye watawaita, ili kwenda kukaa pamoja na kuzungumzia hilo suala.

Grand Malt ilianza udhamini wake mwaka 2012 ambapo mwaka huu inamaliza msimu wake ambapo tokea kuanza kwa kipindi imeshafikia udhamini wa zaidi ya Sh milioni 240.



CHANZO: HABARI LEO

About Unknown

0 comments:

Powered by Blogger.