VPL

Vibangwa vya VPL 2010/2011

aamsuni:

Ligi kuu ya Tanzania bara (vpl) 2010/11 ilifikiwa tamata jana ambapo yanga waliibuka mabingwa wakati Mrisho Ngassa akiwa mfungaji bora. Yafuatayo ni matukio yaliyotokea katika msimu wa 2010/11.
IMANI NA KASEJA.
Mashabiki wa Simba na soka la bongo walikuwa na imani kubwa Kaseja katika ulinzi wa goli. Kaseja ambaye msimu huu alianza kwa kuuguza jeraha la kidole amepoteza imani kwa mashabiki wake.
Mzunguko wa kwanza alikuwa vizuri mpaka kuisaidia Kilimanjaro Stars kutwaa kombe la Tusker na kuibuka kipa bora wa mashindano.
Jinamizi lililo wakumba makipa wengine wa stars liliibuka kwa Kaseja Mapema Mwaka huu kule misri alipotunguliwa tano na kisha kuja kutunguliwa tatu na Azam fc. Tangu hapo Kaseja akawa kaseja mpya ambaye alikuwa anafungwa magoli ya kizembe mpaka msimu unakwisha.
MASHABIKI WA YANGA NA SIMBA KUUNGANA.
Mashabiki wa yanga na simba walikusanya nguvu, kuakisha azam inapoteza mwelekeo, kwa kuwazomea kila wanapoteremka uhuru.
Ni nadra sana kukuta mashabiki wa yanga na simba kuingia uwanjani kwa dhamira ya kuizoofisha timu moja katika mchezo husika.
PRESHA YA AZAM FC.
Azam fc ilianza ligi kwa kususua kabla ya kuwa tishio katika mzunguko wa pili na kuwapa kiwewe wakongwe Simba na yanga kwa kupata matokeo ya uhakika kila inapoteremka dimbani.
Hata ivyo ikaja ikaambulia nafasi ya tatu ya ligi kuu.
GAUDENCE MWAIKIMBA.
Kila mdau alikuwa kamsahau Mwaikimba aliyetamba na Ashanti Utd na kuja kupotea Yanga.
Mwaikimba alitemwa yanga na kusajiliwa na Prisons ya mbeya ambako alishindwa kungara na timu hiyo kushuka daraja. Msimu ulioisha Mwaikimba alisajiliwa Kagera Sugar na ndipo alipo rejesha kiwango chake na kuwa mwiba wa kuotea mbali baada ya kufukuzana na Ngassa.
MRISHO NGASSA NA MUSSA MGOSI.
Ngassa alileta gumzo katika usajili wake wa kutua azam fc akitokea yanga.
Nusu ya magoli ya Azam fc msimu yametokana na Mrisho Ngassa na nnje ya hapo kaibuka mfungaji bora. Ni nadra sana kukuta mchezaji anawatengenezea nafasi nyingi wenzake na pia anaibuka kinara wa wa ufungaji.
Wakati Ngassa akiendelea kungara huku mpinzani wake Mussa Mgosi alieibuka mfungaji bora msimu wa 2009/10 akishindwa kungara.
HONGO.
Timu ya simba kupitia kwa mchezaji wake wazamani Ulimboka waliingia katika shutuma ya kutaka kumuonga kipa wa mtibwa Sugar, Shabani kado, katika pambano baina ya simba na mtibwa sugar lililo chezwa jamhuri Morogoro.
Kipa wa Azama mburundi Vladamir alituhumiwa kuhijumu azam fc katika mechi ya azam na yanga ambayo ilipoteza matumaini kwa azam kuchukua nafasi mbili za juu, huku ikifumua uhai wa ubingwa kwa azam fc.
VURUGU.
Katika pambano la yanga na Kagera sugar lililo pigwa jamhuri Morogoro lilitoa vurugu ambalo lilipelekea kocha wa kagera sugar kujeruhiwa.
Yanga walikutwa na hatia ya kuaribu baadhi ya vifaa vya uwanja wa majimaji katika pambano la yanga dhidi ya majimajii
CCM KIRUMBA.
Katika misimu hii miwili uwanja wa ccm kirumba umebahatika kuchezewa mechi za mwisho wa ligi kuu. huku michezo yote hiyo magoli yake huingia kipindi cha pili, na hicho ndicho kilichotokea jana.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.