judo

Ukata JATA wakwamisha kambi Zanzibar

Elizabeth John

UKATA unaokikabili Chama cha Judo Tanzania (JATA), umesababisha chama hicho kushindwa kupeleka wachezaji wa timu ya taifa katika kambi ya pamoja iliyoandaliwa na chama cha mchezo huo visiwani Zanzibar (ZJA).

Kambi ya pamoja ya judo, imeanza wiki iliyopita katika ukumbi wa Budo Kan ulioko ndani ya Uwanja wa Amani mjini Zanzibar na ilitarajiwa kuwashirikisha wachezaji zaidi ya 50 kutoka bara na visiwani, lakini sasa inaundwa na wachezaji wasiozidi 25 kutoka Zanzibar.

Kwa mujibu wa Katibu wa JATA, Kashinde Bundala, alisema kuwa endapo wangepata fedha wangewahamisha wachezaji 18 walioko kambini katika Shule ya Msingi Kisutu jijini Dar es Salaam, kwenda katika kambi ya pamoja iliyoanzishwa mjini Zanzibar.

Bundala alisema Zanzibar imeandaa kambi hiyo kwa lengo la kuwapatia mazoezi yenye kiwango wachezaji wote wanaounda timu ya taifa ya mchezo huo inayojiandaa na mashindano mafupi ya kuwania kufuzu michuano ya Olimpiki ya Majira ya Joto 2012.

Naye Makamu Mwenyekiti wa ZJA, Haji Hassan, alithibitisha JATA kushindwa kushiriki kambi hiyo, kwa kuongeza kwa kusema wameandaa kambi hiyo ambayo itafikia kikomo Machi 26, lengo likiwa ni kuungana pamoja ili waweze kupata mazoezi ya ziada kwa ajili ya mashindano hayo.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.