 |
Kamera za Azam TV zikiwa kazini katika mchezo wa kirafiki kati ya Azam FC na Ashanti |
Ligi kuu ya mpira wa miguu Tanzania bara wakati wowote itaanza kurushwa moja kwa moja (live) kupitia kituo cha Televisheni cha Azam (Azam TV).
Azam itarusha ligi hiyo katika muonekano mardadi hautakua na tofauti na
ule wa ulaya, kwani kamera nane za Azam TV zitatumika kurekodi kila
pambano litakalo chezwa.
Kuwepo kwa kamera nane uwanjani, huu ni
wastani wa juu wa idadi ya kamera zinazopaswa kuonyesha kwa ufasaha
pambano lolote la soka ingawa katika mechi za ligi nyingine au michuano
mingine kunakuwa na kamera zaidi za kuonyesha mbwembwe mbalimbali.
 |
Kamera za Azam TV zikiwa kazini katika mchezo wa kirafiki kati ya Azam FC na Ashanti
|
Azam TV walitumia mchezo wa kirafik kati ya Azam Academy na Ashanti United uliochezwa katika uwanja wa Azam uliopo ndani ya Complex ya Azam, FC uliochezwa september tano siku ya Alhamisi kujaribia vifaa vyao vitakavyo kuwa vinatumika kurusha matangazo ya moja kwa moja.
0 comments:
Post a Comment