Katika mchezo huo wa mzunguko wa 22, ulishuhudia Azam FC na Mbao FC zikienda mapumziko wakiwa sare ya bila kufungana huku Azam FC wakipoteza nafasi kadhaa za kujipatia goli.
Katika kipinfi cha pili kila timu ilijaribu kutengeneza nafasi, na Azam Fc kuwa wa mwanzo kutumia nafasi katika dakika ya 63 kujiandikia goli la kuongoza kupitia kwa Iddi Kipagwile aliyeingia kuchukuwa nafasi ya Joseph Mahundi katika dakika ya 62.
Wakati Mbao wakijuilza nini kilicho wa kumba walijikuta wanaruhusu goli la pili katika dakika ya 72 kupitia kwa mtokea benchi Bernad Arthur aliyeingia katika dakika ya 60 kuchukuwa nafasi ya Shaban Iddi, akimalizia kazi nzuri ya Salum Abubakari "Sure Boy".
Wakati Mwadini Ally akiamini na leo atatoka bila ya javu zake kuguswa baada ya kufanya hivyo katika michezo miwili iliyopita, alijikuta anaruhusu nyavu zake kuguswa katika dakika ya 90, mfungaji akiwa Emanuel Mvuyekure, na kupelekea mchezo kumalizika kwa Azam FC kushinda goli 2-1.
Matokeo hayo ya leo yanaifanya Azam FC kusogea mpaka nafasi ya pili wakiwa na pointi 44, na kuishusha yanga ambayo wanataraji kucheza hapo kesho dhidi ya Stand United.
0 comments:
Post a Comment