Timu hiyo ambayo imewahi kushiriki Ligi Kuu ya Tanzania Bara katika msimu wa 2006 na baadaye kushuka daraja imekuwa katika jitihada za kutaka kurejea Ligi Kuu ya Tanzania Bara bila mafanikio kwa kipindi chote.
Akizungumza mmoja wa viongozi wa timu hiyo ambayo ipo mjini hapa kushiriki kombe maalumu lililoandaliwa na Chama cha Soka Dodoma (DOREFA), Kempard Samson alisema wameanza maandalizi mapema ili wafanye vizuri katika ligi inayotarajiwa kuanza hivi karibuni.
Alisema katika kombe hilo la FA, wameifunga Dundee kwa mabao 3-0 hivyo kuzitaka timu zitakazokutana na timu yake kuwa tayari kupata kipigo.
“Tunataka turejee Ligi Kuu ya Tanzania ndio maana tumeanza maandalizi mapema, pia kupitia mashindano ya Dorefa tunatengeneza timu ya ushindi ambayo itarudisha furaha kwa wakazi wa Dodoma ambao wamekosa ligi kuona Ligi Kuu ya Tanzania Bara,” alisema Samson.
0 comments:
Post a Comment