aamsuni
Mshikemshike wa ligi kuu Tanzania bara "VPL" kuendelea leo kwa mchezo mmoja, utakao pigwa katika uwanja wa uhuru jijini Dar es salaam.
Mtanange wa leo utawakutanisha timu mbili zinazotafuta kujihakikishia kuwepo katika ligi kuu msimu ujao. Africa lyon inayoshika nafasi ya nane yenye pointi 19 itawakaribisha timu ya Polisi Dodoma yenye point 17 na ipo katika nafasi ya tisa.
Polisi Dodoma pamoja na Africa lyon bado hawaja jiakikishia kuwepo kwao msimu ujao kutokana na kuwa na tofauti ya pointi nane na yule aliye wa mwisho, ambazo anaweza kuzipata katika mechi nne zilizo salia.
Timu zote zitashuka uwanja kwa lengo la kuvuna point zote 3 ili ijiweke pazuri.
Timu nyingine zinazo chungulia kushuka daraja ni Ruvu Shoting yenye point 15, Maji maji pointi 12, pamoja na AFC iliyopoteza matumaini. Ubingwa wa ligi unagopaniwa na Simba point 38, yanga pointi 39 na Azam point 36.
0 comments:
Post a Comment