Mchangani

Ambani, Mwalala, Sirengo kukipiga simba na yanga

copied from Habari leo

WASHAMBULIAJI raia wa Kenya Boniface Ambani, Benard Mwalala na Mark Sirengo ni miongoni mwa nyota wanaotarajiwa kucheza meshi ya wachezaji nyota wa Simba na Yanga Jumamosi wiki hii Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Mechi hiyo ya hisani imeandaliwa na taasisi isiyo ya kiserikali ya Tanzania Sports Catalyst kwa ajili ya kusaidia watu walioathirika na milipuko ya mabomu iliyotokea katika kambi ya jeshi Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi wa taasisi hiyo , Suleiman Mathew katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam akiambatana na Ofisa Habari wa Simba Clifford Ndimbo na yule wa Yanga Louis Sendeu alieleza kuwa maandalizi yanaenda vizuri. Ndimbo alitaja nyota wa zamani ambao wataunda kikosi hicho cha Simba ambao watakuwa chini ya Kocha Abdallah Kibaden ‘King’ kuwa ni Mohamed Mwameja, Kelvin Mhagama, Issa Manofu, Aboubakar Kombo, Said Sued, Boniface Pawasa, Ramadhan Wasso na Barnabasa Sekelo. Wengine Suleiman Matola, Iddi Selemani, Yusuf Macho, Abdul Mashine, Kamba Luffo, Shekhan Rashid, Bakari Iddi, Steven Mapunda, Wilfred Kidau, Shauri Iddi, Mrisho Moshi, Thomas Kipese, Dua Said, Emmanuel Gabriel, Bita John, Ulimboka Mwakingwe, Mark Sirengo na Madaraka Selemani ‘ Mzee wa Kiminyio’. Kwa upande wa Yanga ambacho kikosi chake kipo chini ya kocha Kennedy Mwaisabula kinaundwa na Peter Manyika, Mfaume Athumani, Ismail Suma, Mwanamtwa Kihwelo, John Mwansasu, Bakari Malima, Mzee Abdallah, Omary Kapilima, Banza Tshikala, Anwara Awadh Shaaban Ramadhani na Salvatory Edward. Wengine ni Abdul Maneno, Ally Mayai, Waziri Mahadhi, Edibilly Lunyamila, Ephraim Makoye, Iddi Moshi, Aaron Nyanda, Mohamed Hussein ‘Mmachinga’, Akida Makunda, Ally Yusuf ‘Tigana’ na nyota kutoka Kenya Bernard Mwalala, Boniface Ambani na Edwin Mukenya ambao watajiunga na wenzao Alhamisi kwenye mazoezi ambayo yanaendelea kwenye uwanja wao wa Kaunda. Viingilio katika mchezo huo ni Sh 10 ,000 kwa jukwaa la V.I.P A, sh. 5 000 V.I.P B na V.I.P C sh. 3 ,000 na kwa wale watakaokaa kwenye viti vya rangi ya Chungwa watatakiwa kulipa Sh 2 ,000 na vile vya bluu na kijani Sh 1 ,000.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.