VPL

YANAGA YAICHAPA 3 KAGERA, WABAKISHA 3 KUIKAMATA SIMBA SC


Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya vodacom Yanga wameendelea kuifukuza Simba SC katika mbio za ubingwa baada ya leo kufanikiwa kupunguza tofauti ya pointi kutoka 6 mpaka kufikia 3, kufuatia kuwafunga Kagera Sugar goli 3-0.

Katika mchezo huo wa ligi kuu ya vodacom uliochezwa katika uwanja wa Taifa, ulishuhudia timu zikienda mapumziko wakiwa sare ya bila kufungana.

Baada ya dakika takribani 700 mshambuliaji wa Yanga aliyesajiliwa msimu huu akitokea Simba SC Ibrahim Ajib alifanikiwa kupata goli hii leo likiwa ni goli la kwanza kwa Yanga SC katika dakika ya 53 kwa mkwaju wa penati.

Yanga waliandika goli la pili katika dakika ya 77 kupitia kwa Yusuph Mhilu na goli la tatu likifungwa na Juma Shemvuni katika dakika ya 88 ya mchezo na kupeleka mchezo kumalzika kwa yanga kushinda goli 3-0.

Ushinfi huu leo kwa Yanga SC umaifanya Yanga SC kufikisha pointi 43 baada ya kucheza michezo 20 sawa na Simba SC wenye pointi 46, huku Azam FC iliyocheza michezo 21 ikiwa ya tatu na point 42.

Kwa upande wa Kagera sugar wanao nolewa na kocha Mecky Mexime hali imeendele kuwa mbay kwa wakiabikwa na point zao 18 wakiwa katika nafasi ya 14 baada ya kucheza michezo 21.

About dada

0 comments:

Powered by Blogger.