VPL

Azam fc kuitafuta Yanga

aamsuni
Azam fc inateremka katika uwanja wa uhuru kuwakabili wakata miwa wa Turiani Mtibwa sugar, katika mweendelezo wa ligi kuu ya vodacom.
Azam fc wanateremka uwanjani kusaka point zote tatu, ambazo zitamuweka vizuri kabla ya kucheza na Yanga hapo machi 30. Endapo azam fc ikishinda leo itakuwa na tofauti ya point moja na yanga ambayo iko nafasi ya pili.
Azam fc itakosa huduma ya mkenya Ibrahim Shikanda pamoja na Ibrahim Mwaipopo katika mchezo wa leo unaotarajiwa kuwa na uvutani.
Mtibwa sugar itaingia uwanjani wakiwa na kumbukumbu ya kichapo cha magoli manne kutoka kwa azam walipokutana katika mzunguko wa kwanza pala Manungu complex. Safu ya ulinzi ya mtibwa sugar itakuwa na kazi ya ziada kuizuia safu ya ushambuliaji ya Azam fc inayoongozwa na Ngassa.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.