aamsuni
Azam fc imepata sare ya pili mfululizo hapo jana, alipo kutana na Mtibwa sugar. Azama fc inayoinyemelea yanga kwa ukaribu imejikuta ikishindwa kupunguza tofauti ya point baina yake yeye na yanga kabla hawaja kutana machi 30.
Katika mpambano huo wajana ambao ulikuwa na msimko wa aina yake, huku mashabiki wa yanga wakiishangilia mtibwa sugar, walienda mapumziko bila ya nyavu kutikiswa.
Kipindi cha pili kilianza kwa azam fc kupata bao kupitia kwa John Boko mnamo dakika 53. Goli hilo liliwaamsha mtibwa na kuanza kulisakama goli la Azam fc na hatimaye kusawazisha goli hilo.
Mchezaji khari zaidi nchini, Mrisho Ngassa alizidi kuonyesha uimara wake katika kufumania nyavu baada ya kufunga goli zuri. Hata hivyo hilo goli alikudumu kwani mtibwa sugar walisawazisha goli hilo kupitia kwa Shaban Nditi, na kupelekea mchezo uishe kwa sare ya mbili kwa mbili.
Mtibwa sugar imebaki katika nafasi yake ya nne ikiwa na point 31 huku azam akibakia katika nafasi ya tatu akiwa na point 37 nyuma ya point 3 kwa yanga na point 7 kwa anayeongoza ligi simba sc. Kila timu imebakisha michezo mitatu, huku azam fc ikitarajiwa kushuka uwanjani machi 30 kuikabili yanga, mchezo ambao ndio utakao amua kama azam atapata nafasi ya kuiwakilisha nchi au la.
Huku hayo ya kijili mbio za kuwania ufungaji bora unazidi kushika kasi, ikiwa inaongozwa na Mrisho Ngassa mwenye magoli 13 akifuatiwa kwa ukaribu na Gaudienc Mwaikimba mwenye magoli 12.
0 comments:
Post a Comment