vilabu

Banka na Kanoni waenguliwa Lubumbashi

aamsuni

Mohammed Banka na Salum Kanoni hawamo kwenye msafara wa Simba ulio ondoka Dar es salaam leo saa moja asubuhi kuelekea Lubumbashi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC). Wachezaji wengine ambao awamo kwenye msafara huo ni Uhuru Selemani, Joseph Owino, Faraji Kabali, Abdulhalim Humoud, Kelvin Charles, Hillary Echesa na Aziz Gila.
Msafara huo wenye wachezaji 18, benchi la ufundi lenye watu 4, na wanne wengine kutoka kwa Friends of simba, unaongozwa na Mwenyekiti wa klabu hiyo, Ismail Rage.
Wachezaji walio ondoka ni Juma Kaseja, Ally Mustapha, Haruna Shamte, Juma Jabu, Juma Nyoso, Kelvin Yondani, Jerry Santo, Meshack Abel, Amir Maftah, Amri Kiemba, Shija Mkina, Mussa Mgosi, Mbwana Samatta, Emmanuel Okwi, Patrick Ochan, Rashid Gumbo, Ally Ahmed na Nico Nyagawa.
Simba kesho watacheza na TP Mazembe huko Lubumbashi mchezo wa hatua ya kwanza ya ligi ya mabingwa Africa.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.