zanzibar

Dr Shein kuongoza Harambee

aamsuni
Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Dk. Ali Mohammed Shein, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika hafla ya kuichangia soka la Zanzibar, itakayofanyika kwenye ukumbi wa Zanzibar Beach Resort visiwani humo Machi 26.
Mkurugenzi wa Future Century Sports Limited, Hellen Masanja, alisema “Tunahitaji wadau wa kudumu wa kuliendeleza soka la Zanzibar, ndio maana tumelenga kuwaita ili waje wakae nasi katika kuendeleza soka letu la visiwani."
Masanja aliendelea kusema mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es salaam, tukio hilo litawakutanisha wadau mbalimbali kwa lengo la kukusanya dola laki mbili ambapo wataongozwa na Rais Shein na litarushwa na kituo cha Super Sports Africa kupitia DSTV na kuonekana kwenye nchi 48 za Afrika.
Kwa upande wake, meneja wa mradi huo kutoka Future Century Sports Limited, Martha Enock, aliwataja wadau mbalimbali watakaofanikisha hafla hiyo kuwa ni pamoja na Benki ya Watu wa Zanzibar, Shirika la Bima la Zanzibar (ZIC), Mamlaka ya Bandari Zanzibar (ZSSF), Zantel, Multchoice Tanzania, Vodacom, Radio na Clouds Tv, Seaforth Agency, Moreover, Tanzania Distilleries, Zanzibar Beach Resorts, New Africa Hotel, Explore Zanzibar, METL na Anver Rajpar ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya uchangiaji Dar es Salaam.
Soka la Zanzibar alinamdhamini na hivyo kupelekea kuendelea kuzorota kadri ya miaka inavyo kwenda na mda mwingine ligi kuu zanzibar kukwama kufanyika.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.