copied from mwanaspoti
Julius Patrick Mrope ni mchezaji wa zamani wa Simba iliyomuacha bila sababu na kumfanya abaki uraiani kwa mwaka mzima hadi Nizar Khalfan anayeichezea White Caps ya Canada alipomshauri kujiunga na Manyema Rangers ikiwa Daraja la Kwanza.
Katika mahojiano na Mwanaspoti, Mrope anasema: Utake usitake klabu za Simba, Yanga na Azam FC kwa sasa ndizo zinazotoa watu kimaisha kutokana na maslahi ambayo wachezaji wanayapata katika klabu hizo. Siyo kwamba naziponda timu nyingine, ukweli unabaki kuwa ziko juu kimaslahi.
Mtibwa Sugar ninayoichezea sasa naweza kusema ni sawa na baba au mama yangu mzazi baada ya kunitoa huko na kunifikisha hapa nilipo sasa natambulika, nimerudi tena, anaeleza Mrope, ambaye hivi karibuni aliitwa kwenye kikosi cha Taifa Stars. Wanasoka huwa tunaangalia maslahi kwa kuwa ndiyo kazi ambayo tumeichagua, anasema Mrope, aliyeichezea Serengeti Boys mwaka 2005 hadi 2006.
Unaposaini kuichezea Simba, Yanga au Azam maslahi unayoyapata ni makubwa huwezi kuyafananisha na timu nyingine, anasema Mrope anayempenda Lionel Messi wa Barcelona ya Hispania. Fedha unazozipata katika usajili wao kama uko makini zinaweza kubadilisha maisha yako. Ukiachana na fedha za usajili, kwa upande wa mishahara wachezaji wanapata mishahara mikubwa, kuna posho nzuri pamoja na marupurupu mengine.
Wale wachezaji wanaoharibikiwa kimaisha bila shaka hawakuwa makini kutunza walichokuwa wanapata maana unaweza kucheza muda mfupi tu ukatoka, anaeleza Mrope. Lakini pia klabu hizi kubwa zinakufanya kutambulika kwenye ulimwengu wa soka.
Akizungumzia kuachwa kwake na Simba, Mrope anaeleza: Klabu hizi kubwa zina matatizo yake pia, Simba waliniacha bila kuniambia sababu maalumu, anasema Mrope aliyeanzia soka yake akiwa Shule ya Msingi ya Kambarage jijini Dar es Salaam mwaka 2000.
SABABU ZINAZOUA VIWANGO VYA WACHEZAJI
Mrope anasema: Zipo sababu nyingi zinazoua vipaji vya wachezaji wengi, kubwa zaidi ni kulewa sifa mara tu wanapopata umaarufu. Nasema haya kwa sababu mimi pia ni mchezaji na nime
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment