aamsuni
Kipa anae aminika kuwa bora Tanzania Juma kaseja ameungana na makipa wenzake mashuhuru duniani kuulalamikia mpira wa jabulani.
Hilo limekuja baada ya kipa huyo kushindwa kuzuia goli la kwanza la TP Mazembe lililofungwa dakika ya 11 kwa shuti lililompita juu ya kichwa Kaseja, ambaye alitaka kuukamata na ukamshinda.
Lakini akizungumza mjini Dar es Salaam, Kaseja amesema mipira aina ya Jabulani inateleza na hakutarajia kwamba ingetokea hali ile. “Nilikuwa napanga mabeki wangu, lakini hata kabla sijamaliza kuwapanga jamaa wakapiga, hivyo kuja kushtuka mpira huu hapa na nataka kuushika ukawa umeponyoka. “Jabulani si mipira mizuri hasa kwa makipa, hata kipindi cha pili ilitokea hali kama ile, mipira kwa kweli inateleza sana, ni ngumu kwa mtu wa kawaida kuamini. “Unaweza kutoa lawama kwa Kaseja, lakini hali haipo hivyo, makipa wengi wameshazungumzia jambo hili,” alisema Kaseja.
Juni mwaka jana aliyekuwa kipa wa Taifa Stars, Mwarami Mohammed, alilalamikia mipira hiyo baada ya Stars kufungwa mabao 5-1 na Brazil katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, lakini wengi hawakusadiki, hata Shaban Kado aliulalamikia mpira huo baada ya kufungwa goli Moja na Rwanda katika mchezo uliochezwa Kigali wa kufuzu kushiriki michuano ya CHAN.
Mipira hiyo ya jabulani ilianza kulalamikiwa na Enyeama mapema mwaka jana kabla ya makipa wengine akiwemo Julio Cesar, Iker Casillas na Tim Howard kuilalamikia kipindi cha world cup.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment