aamsuni
Kocha mwenye rekodi nzuri nchini Abdallah Kibaden 'Mputa' amekabidhiwa timu ya simba, inayojianda na mpambano dhidi ya mabingwa wa Afrika TP Mazembe.
Kocha wa timu hiyo Phiri alirejea kwao baada ya mchezo wa kwanza wa TP Mazembe na Simba kwa matatizo ya kifamilia. Phiri alitarajiwa kurudi katikati mwa wiki hii ambapo bado ajawasili na simba kufikia uwamuzi wa kumjumuisha Kibaden katika bench la ufundi litakalo ivaa TP Mazembe.
Akizungumza jijini Dar es salaam jana, Mwenyekiti wa Simba, Aden Rage alisema kutokana na udhuru wa kocha huyo, Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo iliyokutana juzi imeamua kumkabidhi timu kocha Kibaden. "Mechi inayotukabili ni ngumu hivyo kamati imeona ni vyema timu akakabidhiwa Kibaden, na hata kama Phiri atarejea nchini basi Mputa atakuwa kocha msaidizi wa timu hiyo, pamoja Amour Awadhi wa Oman atakuwa kocha wa makipa ikiwa ni moja ya mbinu za kuimarisha benchi la ufundi," alisema Rage.
Kibaden aliiongoza timu ya vijana chini ya miaka 17 'serengeti boys' kufuzu kushiriki mashindano ya Afrika lakini timu hiyo ilifungiwa na kushindwa kushiriki. Pia aliiongoza Simba kucheza fainali ya la shirikisho mwaka 1993.
Kibaden ana kazi ya ziada ya kuakikisha Simba inaendeleza wembe wake wa kuwatoa Mabingwa watetezi kila wanapopangiwa nao tangu mwaka 1974.
Mchezo huo wa marudiano utapigwa april 3 katika uwanja wa Taifa na utaanza saa tisa mchana. Wakati mnyama Simba akihitaji magoli mawilio bila ya kuruhusu goli kwenye nyavu zake.
0 comments:
Post a Comment