aamsuni
Beki wa kati wa Mtibwa Sugar, Salum Sued Kusi amemaliza majaribio yake ya wiki mbili na kufanikiwa kufuzu katika klabu ya Ferrovoviario de Nampula ya Msumbiji na anatarijiwa kurejea nchini kesho jumatano.
Kusi anarejea nchini kwa ajili ya mazungumzo na klabu yake ya Mtibwa sugar. Salum Sued Kusi alirejea mtibwa sugar katika dirisha dogo la usajili akitoke Azam fc, iliyo muacha.
Usajili wa Msumbuji unafungwa tarehe 30 machi, wakati ligi hiyo ikiwa teyari imeshaanza tangu machi 6. Kusi ataungana na nyota wenzake wazamani wa timu ya taifa wanaocheza ligi kuu ya Msumbiji ambaye Victor Costa 'Nyumba' pamoja na Mohammed Mwarami.
0 comments:
Post a Comment