copied habari leo
MICHUANO ya ligi ya taifa ngazi ya mkoa wa Shinyanga inayozishirikisha timu 24 kwenye vituo vinne vya Mwadui, Usanda Bariadi na Msumbwe inaendelea kuchukua kasi.
Katika mfululizo wa michuano hiyo kituo cha Bariadi hakuna mchezo uliofanyika baada ya timu za wilaya ya Meatu za Mshikamano na Mwandoya United kushindwa kufika kwenye michezo mitatu zilizopangiwa dhidi ya timu za Carfonia ya Bariadi,Lamadi F.C. na Vijana ya Maswa.
Kutokufika kwa timu hizo kwenye michezo hiyo kulinufaisha wapinzani wao kwa kujipatia ushindi wa chee wa mabao matatu na pointi tatu.
Kwenye kituo cha Masumbwe wilayani Bukombe, timu ya Tulivu ya Mgaya na Cobra ya Masumbwe zilishindwa kutambiana baada ya kutoka sare ya kufungana mabao 3-3, katika mchezo mwingine wa kituo hicho Tulivu na Ushirombo Stars zilitoka sare ya kufungana bao 1-1, Vijana Segese ikainyuka Leopard bao 1-0.
Kwenye kituo cha Mwadui timu ya Mwadui F.C. iliinyuka Ndala Community kwa mabao 5-0, Nguzo nane iliiadhibu Malampaka United ya Malampaka kwa mabao 5-2. Kwenye kituo cha Usanda timu ya Shinyanga United iliitandika Original ya Usanda kwa bao 1-0 katika mchezo mwingine wa ligi hiyo timu ya Ambasada ya Kahama iliichapa Original ya Usanda kwa mabao 2-1.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment