VPL

Majimaji yaivuta Ruvu shooting

aamsuni
Jioni ya leo mkoani Songea kulikuwa na mchezo wa ligi kuu ya vodacom 'VPL', ambapo timu ya majimaji ilimkaribisha Toto Africa katika uwanja wa majimaji.
Katika mchezo huo ambao ulikuwa wa muhimu kwa timu ya majimaji ambayo iko katika harakati za kujinusuru kushuka daraja, ilishuhudia mwenyeji majimaji ikiibuka kidedea kwa ushindi wa magoli mawili kwa moja.
Kutokana na matokeo hayo Majimaji imefikisha point 16, nyuma point moja kwa Ruvu shooting yenye point 17.
Ruvu shooting inatakiwa kushinda michezo yake iliyo salia kama anataka kubakia katika ligi kuu. Endapo ruvu shooting itapoteza michezo yake miwili huku Majimaji wakimfunga simba, itapelekea kushuka daraja kwa Ruvu shooting na hivyo kuungana na AFC ya Arusha.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.