vilabu

Mashambulizi ya mdomo TP Mazembe wametoka

aamsuni
Tanzania tunasifika sana kwa maneno na mipango ya kwenye midomo, huku tukishindwa kuyafanyia kazi yale tunayo ya sema.
Baada ya Mchezo wa Mazembe na Simba, kauli zinazidi kutawala za ushindi kwenye midomo. Hizo kauli singeni kwa wanao fuatilia soka la Tanzania na mara nyingi hizo kauli za kutafuta ushindi mdomoni zimetuasili sana.
Miaka mitatu iliyopita yanga walitoka sare ugenini wa moja moja nchini libya, na kujipa matumaini makubwa ya kupita lakini pale uhuru walijikuta wakipoteza nafasi nyingi hadi penalti walikosa na kujikuta wako nnje ya mashindano.
Mwaka jana ilikuwa kwa upande wa simba ambao walicheza na Hadoud pale Taifa na kuibuka na ushindi wa goli mbili kwa moja. Kama kawaida mipango ya kwenye midomo ikapangwa na kujikuta wanapokea kichapo cha goli Tano kwa moja, huku simba wakishindwa kutumia nafasi walizopata na kujikuta wako nje.
Tabia ya kuzishusha kiwango kwa mdomo timu pinzani ziliendelea kuathiri mpaka timu ya Taifa na kushindwa kufuzu kwenda Sudan 'CHAN' pale walipo kuwa wanarudiana na Rwanda, na zile za AFCON zilizofanyika Ghana hata na zile za Angola ambazo Taifa stars walikuwa na nafasi kubwa ya kufuzu.
Natoa taadhari kwa Simba, TP Mazembe hawafungiki kwa kupiga porojo bali watafungika kwa mipango uwanjani kuwanzi kwa walinzi mpaka washambuliaji kutumia nafasi wanazopata.
Nnje ya hapo tusije shangaa tukipokea kichapo kitakatifu kutoka kwa Mazembe kama kile cha Enyimba. Mazembe si timu ya kawaida kama mnavyo ichukulia na wamepiga hatua ndefu, na timu bora ni ile yenye safu imara na ni wazuri kutumia nafasi wanazopata.
Simba ijipange kutumia kila nafasi wanayoipata, mchezo wa mpira ni mchezo wa makosa, bila ya makosa hamna magoli.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.