aamsuni
Mchezo wa wachezaji walio tamba siku za nyuma katika timu za simba na yanga uliofanyika katika uwanja wa Taifa umeingiza Tsh milioni 13.2. Mchezo huo ulikuwa maalum kwa kukusanya fedha kwa waathirika wa mabomu ya Gongo la mboto.
Fedha hizo zimetokana na mashabiki 10,796 walioingia uwanjani, ambapo kati ya hizo sh. milioni moja zimepangwa kupelekwa kwa waathirika wa mabomu.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Mratibu wa mechi hiyo Seleman Mathew alisema "Baada ya kufanya mchanganuo wa mapato yote kwa kulipa madeni, kuanzia uwanja, maaskari na vitu vingine vyote fedha iliyobakia ni Tsh. milioni 1 ambayo inakwenda moja kwa moja kwa waathirika wa mabomu."
Alisema fedha hizo wanatarajia kukabidhi katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa ajili ya kwenda kuwakabidhi waathirika hao wa mabomu.
Mathew alisema wamepokea mwaliko kutoka mkoani Dodoma, na hivyo simba na yanga watarudiana Aprili 22 au 23 mwaka huu.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment