CAF

Mwanafunzi ni mwanafunzi.

aamsuni
Kocha wa simba Patrik Phiri alikaririwa na mwananchi akisema pambano la leo, nikati ya mwanafunzi na mwalimu. Mwanafunzi akiwa simba wakati mwalimu akiwa Mazembe, lakini alisema pamoja na uwanafunzi wao, watamuangusha mwalimu.
Dakika tisini la pambano likatoa jawabu, la mwanafunzi ni mwanafunzi na wala hana ubavu kwa mwalimu. Baada ya matokeo ya mwisho kusomeka Tp Mazembe 3 simba 1.
Simba ambayo iliadiwa Tsh milion 100 endapo wangeshinda na milioni 50 kama wangetoa sare walijikuta wakisaka mpira kwa tochi katika pambano la leo.
TP Mazembe waliliandama lango la simba kwa dakika 18 za mwanzo na kufanikiwa kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa magoli mawili kwa bila.
Simba ambayo ilikuwa na kazi ya kutafuta mpira walipata goli la kufutia machozi kwa mkwaju wa penalt kupitia kwa Mganda Emanuel Okwi. Mpaka mwisho wa mchezo simba goli moja TP Mazembe goli tatu.

Simba itakuwa na kazi ya kufanya pale watakapo rudiana jijini Dar es salaam baada ya wiki mbili. Simba itaitaji ushindi wa goli mbili bila katika mchezo wa marudiano ili waweze kuifungisha virago TP Mazembe. Kinyume na hapo itakuwa ndio mwisho wa simba katika klabu bingwa afrika na kufunika ahadi ya Phiri.

About kj

0 comments:

Powered by Blogger.