aamsuni
Mashindano ya NSSF yanayo shirikisha vyo vya habari Tanzania yalianza kutimua kasi hapo machi 19, na jana kuendelea kwa mchezo baina ya Mwananchi FC na Uhuru publication na ule baina ya radio kheri na habari zanzibar.
Mchezo wa mwananchi fc na uhuru publication uliofanyika katika viwanja vya chuo kikuu cha uwalimu DUCE, zilitoka sare ya goli moja kwa moja. Mwananchi walikuwa wa kwanza kuandika goli kupitia kwa Ibrahim Masoud kwa kombora la mbali lililo mshinda kipa wa Uhuru katika dakika ya 39. Goli hilo lilidumu mpaka mapumziko.
Kipindi cha pili Mwananchi FC ilijikuta ikipoteza nafasi nyingi huku wapinzani wao wakitumia vizuri nafasi waliyoipata kusawazisha goli kupitia kwa Fred Mpokigwe na hivyo kupelekea mchezo uishe kwa sare ya moja kwa moja.
Katika mchezo mwingine, Radio Kheri ilitoka suluhu na Habari Zanzibar, mchezo uliofanyika kwenye Viwanja vya TCC Chang'ombe.
0 comments:
Post a Comment